Fabievents ni suluhisho ya mandalizi ya sherehe zote Tanzania
Kama wewe ni Bwana harusi au Bibi harusi mtarajiwa zijue mbinu.
• Kama unatarajia kuchangisha kwenye harusi yako hakikisha unachangia harusi za wengine pia, na hata kuwa kwenye kamati ya mandalizi, inapofika zamu yako kufanya harusi tayali unakuwa na ile network ya watu kadhaa. Ukifanya hivyo Zaidi ya mara moja inakupa wigo mkubwa wa kuwa na network nzuri tena ya wachangiaji wa sherehe, Kujichanganya na matukio ya kijamii pia ni njia nzuri yakuzidi kupata marafiki wa faida, ikiwemo hata kumtembelea ndugu/rafiki ambaye anaumwa.

• Chukua namba za simu za marafiki wako uliowasave na wanakujua, Kisha wambie wakutumie namba za marafiki wengine ambao umepotezana nao inaweza kuwa ulisoma nao sehemu Fulani au uliwahi fanya nao kazi.

• Andika namba za ndugu zako wanaokujua ukishamaliza, wambie wazazi/walezi wako wakusaidie kukupa namba za simu na majina ya ndugu ambao wewe unaweza kuwa huwajui au haupo karibu nao, kupitia huu mchakato utakua umefikisha wadau wengi kushiriki kwenye mandalizi ya harusi yako.


• Majina na namba za simu ulizopata unaweza kuwa umeandika kwenye excel kisha ndo ufanye upload au umesave moja kwa moja ndani ya Fabievents, ndani ya Fabievents unaweza tengeneza groups mbali mbali kulingana na aina wa watu wako ulionao kuna wengine huwezi wakutanisha pamoja kutokana na ratiba zao au status zao.

• Siyo lazima kutengeneza kadi ya mchango ambazo zipo printed, Unaweza tengeneza softcopy na ukashare kwenye groups za WhatsApp achana na mambo yakizamani kwamba mtu lazima mpelekee kadi ya mchango mtu kama anania yakutoa mchango atatoa tu maana atakuwa anakumbushwa tarehe ya harusi kupitia fabievents cha kufanya ni kumuweka tu ndani ya fabievents mapemaaa.

• Fanya kikao cha kwanza kwa kuwatumia ujumbe wa kuwataarifu kwamba mimi ni mtu fulani nitafanya kikao cha kwanza cha harusi yangu siku fulani . Kama hutoweza kufika siku ya kikao cha kwanza naomba uniambie ahadi yako kupitia sms ama kupiga simu. Kwakufanya hivyo utapata adahi zote za ambao watakuja kwenye kikao na ambao hawatakuja. Pia uzuri mwingine ni kwamba wakati unatuma ujumbe utaenda na jina la mpokeaji moja kwa moja atajua yeye ndo mlengwa. Jamani Fabievents ni raha sana hahahahahha yani navyoendelea kusoma naona kama nishapunguza stress za michango hahahhaha kweli hii ni your event solutions.


• Ni vema ukifanya mandalizi ya harusi kabla ya miezi mitano hii ni kwa upande wa ambao unatarajia kuomba michango ila kwa upande wako lazima uwe umejipanga mapema. Kwa nini tunasema uwe umejipanga mapema inaweza kuwa aina ya watu wako wakatuma michango kwenye deadline siku tatu au mbili kabla na ujue unatakiwa uwe ushalipia kama ukumbi na baadhi ya watoa huduma.

• Upande wa watoa huduma “USIANGALIE BEI NAFUU, ANGALIA UBORA WA MTOA HUDUMA KWANZA”

Usihau kushare hii link kwa kwengine.